HISTORIA
YA KIKUNDI CHA ANGAZIA MEMA
1.0. JINA LA KIKUNDI : ANGAZIA MEMA
KUANZISHWA : 2012
MAKAO MAKUU : Kawe,
Kinondoni Dar es Salaam TZ
Mawsiliano
SIMU : 0689654599
BARUA PEPE : zagragroup@outlook.com
P.O.BOX : 31902
2.0 Mahali kikundi kinapatikana.
Kikundi kinapatikana Mtaa
wa ukwamani. Mkabala na ofisi ya mtendaji wa kata ya kawe.Jilani kabisa na soko
la kawe.
3.0
KUANZISHWA
KWA KIKUNDI
Kikundi
kilianzishwa Mwaka 2012 kwa jina la Tegemea Mema kama kikundi cha kuweka na kukopa. mwaka 2018 kikundi
kikasajiliwa chini ya halimashauri ya manispaa ya Kinondoni kwa jina la ANGAZIA
MEMA, na kupewa hati ya kuandikishwa, kuwa kikundi cha ujasiriamali na maendeo
katika nyanja ya kibiashara na elimu katika ngazi ya ujuzi. Hii ni kuwezesha kikundi
kufikia malengo yake. Kikundi hii cha angazia mema ni endelevu.
B. Malengo ya ANGAZIA MEMA
(i)
Inaunganisha jamii kua kama familia moja katika
elimu ya ngazi ya ujuzi , kujengea Jamii mazoea ya kutumia elimu iliyopo
kujiajiri na kujiingizia kipato ili kupunguza
wimbi la vijana tegemezi.
(ii) kujiandaa na wakati ujao Kwa Kuanzisha Shughuli za Ujasiriamali ambazo zaweza
kutoa Ajira na maendeleo kwa Jamii
(iii)
Kuanzisha miradi ya maendeleo yenye lengo la kuhakisha kikundi kina
uwezo wa kutekeleza shughuli zake.
(iv)
kujikita katika Mpango wa Rasilimali za
Biashara,Usimamizi wa Uhusiano wa Vijana, WANAWAKE na walemavu katika maendeo,
Usimamizi wa Maudhui ya Biashara ,Miundombinu ya Biashara, Uchanganuzi wa
Biashara na Mafunzo na Uwezeshaji.
4.0 NAMBA YA USAJILI
Kikundi
Kimesajiriwa na idara ya maendeleo ya jamii ya Halmashahauri ya Wilaya ya
Kinondoni kwa Nambari. KMC/GGR/10858
5.
WANACHAMA
Kikundi
cha angazia mema kina Wanachama wa jinsia zote ambapo idadi kubwa ya wanchama
wake ni wanawake. idadi ya wanachama wake wote ni therasini kama taratibu za
vikundi vya vicoba zinavyo eleza. Pia wanachama wa angazia mema ni watu
walielimishwa vizuri na wakapata uelewa juu ya utunzaji na uendesha wa shughuli
za kikundi kwa maendeleo ya familia zao na jamii kwa ujumla .
‘Kila
mwanachama ni kiongozi katika nafasi yake.’’
hii ni kauli mbiu ya kuwajenga wanachama wake ili kuwa wakundumu na endelevu kuyaikia
malengo yao ya kimaisha.
6.
MAENDELEO YA KIKUNDI
Kikundi
cha angazia mema kina maendeleo makubwa yanayo endana na umri wa kikundi
tangu kianzishwa kwake. Maendeleo ya kikundi ni kama iuatavyo.
1.
MIRADI.Kikundi
kimefanikiwa kumiliki shamba la hekari 10 huko vigwaza wilaya ya chalinze
ambalo ni kama mradi wa pamoja kama mwanzo wa Biashara ya uuzaji aridhi(vinjwa na
mashamba.
2.
MAPATO.
Kikundi kinakusanya makadilio ya mapato ya ndini TZS Mil. 60,000,000 hadi Mil. 63,000,000/=kwa
mwaka Tangu wanachama kuelimika.
3.
MIKOPO.
Kikundi kina aina mbili ya Mikopo yaani Mkopo wa Biashara na mkopo wa jamii, Mkopo wa biashara
hutolewa kwa kutozwa Ziada ya mkopo (riba) mkopo wa Jamii hutolewa Basipo
kutozwa riba.Kikundi kimefikia kutoa mkopo wa biashara wa TZS 18,000,000 na
Kuendelea kwa mwanachama mmoja mmoja tangu mwaka 2018, na wanachama wote ni wadaiwa. Namna ya utoji mikopo Soma
katiba ya kikundi.
4.
GAWIO LA FAIDA.
Kikundi kimefikia kutoa gawio la faida kiasi cha TZS 1,475,000 Kwa mwanchama aliye
na umiliki wa hisa nyingi ambapo mwenye Umiliki wa hisa chache Hupata si chini ya
kiwango TZS 300,000 Kwa mwaka, Hizi nitakwimu za mwaka 2019-2020.
5.
MISAADA.
Kikundi kimetenga Tzs 500,000/=Kwa kila mwanachama kumhudumia katika majanga ya
kila siku (ugonjwa,Misiba nk) kwa mwaka mzima. Pia kikundi kimefanikisha
kumuwezesha kila mwanchama kuwa na bima ya afya.
6.
USHAWISHI.
Kikundi kimfeanikiwa kuzalisha vikundi vingine vitano ambavyo bado ni vichanga.
Kwa ajili ya kuinua jamii yote kutoka katika dimbwi la utegemezi.
7.
MALENGO ENDELEVU. Kikundi
kina mikakati ya kumiliki biashara nyingi zikiwemo biashara ya usafirishaji na
miradi ya uwekezaji wa aridhi ya Pamoja.
Pia tunamikakati ya kuinua Maisha ya mwanachama mmoja mmoja kuikia uchumi
unaolidhisha
7.0.
PONGEZI
Kikundi hii kimeweza
kusimama na kukua kwa muda wote kutokana na viongozi wanaojitole kwa kadri
wawezavyo kupigania kikundi kwa muda wao wote na nguvu na kifikra. Pamoja na
ushilikianao mkubwa wanao upata kutoka katika serikali na wanachama.
0 Comments