Mjue John Pemberton:
Mwanzilishi wa Coca-Cola, Kinywaji Maarufu Zaidi Dunia Nzima. "Wakati dunia ikiwa na changamoto ya kupata kinywaji kitakachopendwa na wengi, John Pemberton alikuwa akijitengenezea dawa ya kujitibu mwenyewe maradhi yake bila kujua anatengeneza kinywaji cha kipekee kinachopendwa duniani leo hii" Na hii ndiyo hadithi yake.
Dr. John Stith Pemberton alizaliwa mwaka 1831, huko Knoxville, Georgia, Marekani. Alikulia Georgia, ambapo alionesha hamu kubwa katika masuala ya tiba na dawa. Aliingia Chuo cha Tiba cha Southern Botanico Medical College huko Macon, Georgia, ambako alipata elimu ya udaktari wa mimea na dawa za kienyeji. Baada ya kuhitimu, alianza kazi kama mfamasia na mtaalamu wa mimea. Katika maisha yake, Pemberton alikuwa akitengeneza vinywaji na madawa mbalimbali ya kienyeji kwa lengo la kusaidia watu waliokuwa wakikumbwa na magonjwa tofauti. Pemberton alihamia Columbus, Georgia, ambapo aliendesha duka lake la dawa na kuanza kufanya majaribio ya kemikali mbalimbali. Huko Columbus, alianza kutengeneza vinywaji vya dawa kwa ajili ya kuondoa maumivu na shida mbalimbali za kiafya.
Katika
miaka ya 1860, Pemberton alipata jeraha kali kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe
ya Marekani (American Civil War) alipojihusisha na mapambano kama sehemu ya
Jeshi la Muungano. Baada ya kujeruhiwa, alianza kutumia morphine ili
kupunguza maumivu, lakini taratibu akaanza kuwa addicted na dawa hiyo. Kutokana
na hili, alianza kutafuta tiba mbadala ambayo ingemsaidia kupunguza utegemezi
wa morphine na kuondoa maumivu. Ndipo alipoanza kufanyia kazi project yake ya
kutengeneza kinywaji cha dawa ambacho kingemsaidia kutuliza maumivu.
Alitengeneza mchanganyiko wa mimea, ambao aliuita "French Wine Coca,"
kwa kutumia majani ya coca (ambayo yana kemikali ya asili ya cocaine), kokwa za
kola ambazo zina kafeini na akaongeza wine kidogo kwa ajili ya radha. Lengo
lake kuu lilikuwa ni kutafuta tiba ya maumivu ya kichwa, uchovu, na msongo wa
mawazo.
Katika miaka ya 1860, Pemberton alipata jeraha kali kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani (American Civil War) alipojihusisha na mapambano kama sehemu ya Jeshi la Muungano. Baada ya kujeruhiwa, alianza kutumia morphine ili kupunguza maumivu, lakini taratibu akaanza kuwa addicted na dawa hiyo. Kutokana na hili, alianza kutafuta tiba mbadala ambayo ingemsaidia kupunguza utegemezi wa morphine na kuondoa maumivu. Ndipo alipoanza kufanyia kazi project yake ya kutengeneza kinywaji cha dawa ambacho kingemsaidia kutuliza maumivu. Alitengeneza mchanganyiko wa mimea, ambao aliuita "French Wine Coca," kwa kutumia majani ya coca (ambayo yana kemikali ya asili ya cocaine), kokwa za kola ambazo zina kafeini na akaongeza wine kidogo kwa ajili ya radha. Lengo lake kuu lilikuwa ni kutafuta tiba ya maumivu ya kichwa, uchovu, na msongo wa mawazo.
Watu
wakaanza kuvutiwa na dawa hiyo, mauzo yakaanza kwenda vizuri na faida ikaanza
kuonekana. Hata hivyo, kwa upande wa Pemberton, furaha haikuwa kubwa kwani
alikuwa akikumbwa na matatizo makubwa ya afya na kifedha. Alikuwa akiteseka
kutokana na saratani ya tumbo na alikuwa addicted to morphine, hali ambayo
ilizidi kumtesa na kuathiri afya yake kwa ujumla. Kutokana na uhitaji mkubwa wa
fedha, Pemberton alianza kuuza kidogo kidogo sehemu ya haki miliki za Coca-Cola
kwa washirika mbalimbali, na hatimaye alimaliza kuuza haki zake zote kwa
mfanyabiashara anayeitwa Asa G. Candler mwaka 1888. Pemberton aliendelea
kuteseka na maradhi yake hadi pale alipofariki dunia mnamo Agosti mwaka 1888
akiwa na umri wa miaka 57.
Asa
Candler aliona fursa kubwa katika Coca-Cola, na kwa kuona maajabu ya kinywaji
hiki, alijua kuwa alikua na bidhaa yenye uwezo wa kuvuma. Mwaka 1892,
alianzisha rasmi kampuni ya Coca-Cola, akijikita zaidi kwenye mikakati ya
kibiashara. Candler alitumia mbinu za kipekee katika masoko na matangazo,
akianzisha kampeni maarufu ya kutoa kuponi za glasi ya bure. Alijitahidi
kuhamasisha watu kwa kuweka matangazo ya Coca-Cola kwenye kalenda, saa za
ukutani, na kadi za biashara, hali iliyochochea umaarufu wa chapa hiyo. Kwa
ujanja wake wa kibiashara, Candler alihakikisha kuwa Coca-Cola inakuwa jina
maarufu na linaloaminika kote Marekani. Mwaka 1894, mfanyabiashara mmoja wa
kutengeneza na kuuza chupa, Joseph A. Biedenharn, alimfata Asa Candler na
kumshauri kwamba kama angependa bidhaa yake ifike mbali zaidi, ingekuwa bora
abadilishe mtindo wake wa uuzaji. Badala ya kuuza kwa glasi na madumu,
alimshauri kwamba angeuza kwa chupa. Lengo la Biedenharn lilikuwa kumsaidia
Candler kuongeza wigo wa soko na kufikia wateja wengi zaidi, kwani aliona
kwamba chupa ingemsaidia kufikisha Coca-Cola kwa urahisi na kwa ubora.
Asa
Candler alikubaliana na wazo hilo, na alipoanza kuweka Coca-Cola kwenye chupa,
mauzo yake yaliongezeka kwa haraka, na aliona kuwa bidhaa yake inafika kwa watu
wengi zaidi. Hata hivyo, changamoto mpya ilijitokeza: Bidhaa ya Coca-Cola ikawa
haiwafikii wateja wotevkwa wakati. Candler alipoona changamoto hii, aliona ni
muhimu kushirikiana na makampuni ya usambazaji ili kumaliza tatizo hilo.
Alishirikiana na Benjamin Thomas na Joseph Whitehead, ambao wao walikuwa na
kampuni ya usambazaji bidhaa tu. Ushirikiano huu kati ya makampuni haya matatu
yalileta matokeo mazuri sana katika historia ya Coca-Cola, kwani sasa bidhaa
hiyo ilikua inawafikia wateja nyumbani kwao kiurahisi na kwa muda sahihi, hivyo
ilichochea sana umaarufu wake duniani kote.
Baada
ya kufanikiwa kuweka Coca-Cola kwenye chupa na kusambaza bidhaa hiyo kwa wingi,
Asa Candler alikutana na changamoto ya ushindani kutoka kwa makampuni mengine
yaliyojaribu kuiga bidhaa yake. Ili kulinda na kuimarisha chapa, Candler
alibadili muundo wa chupa ya Coca-Cola na mwaka 1915 alianzisha chupa maarufu
ya "Contour Bottle," yenye umbo la kipekee. Chupa hii
ilitambulika mara moja na kuifanya Coca-Cola kuwa alama maarufu, huku ikimzuia
vyema Coca-Cola dhidi ya washindani. Mbinu nyingine ya kipekee iliyosaidia
kuvutia wateja ilikuwa ni kampeni ya Christmas. Candler aliona fursa ya
kutumia likizo ya Krismasi ili kuongeza umaarufu wa Coca-Cola. Walibadilisha
picha ya Santa Claus wakamuweka akinywa Coca-Cola, jambo lililovutia
wateja na kuifanya Coca-Cola kuwa sehemu muhimu ya sherehe za Krismasi.
Matangazo haya yalionyesha Coca-Cola kama kinywaji kinachofaa kwa familia
wakati wa sikukuu hi ilipelekea bidhaa hiyo kupedwa zaidi na watu na kuingiza
mauzo zaidi na zaidi kwa Kampuni ya Coca-Cola.
Baada
ya kufanikiwa kuweka Coca-Cola kwenye chupa na kusambaza bidhaa hiyo kwa wingi,
Asa Candler alikutana na changamoto ya ushindani kutoka kwa makampuni mengine
yaliyojaribu kuiga bidhaa yake. Ili kulinda na kuimarisha chapa, Candler
alibadili muundo wa chupa ya Coca-Cola na mwaka 1915 alianzisha chupa maarufu
ya "Contour Bottle," yenye umbo la kipekee. Chupa hii
ilitambulika mara moja na kuifanya Coca-Cola kuwa alama maarufu, huku ikimzuia
vyema Coca-Cola dhidi ya washindani. Mbinu nyingine ya kipekee iliyosaidia
kuvutia wateja ilikuwa ni kampeni ya Christmas. Candler aliona fursa ya
kutumia likizo ya Krismasi ili kuongeza umaarufu wa Coca-Cola. Walibadilisha
picha ya Santa Claus wakamuweka akinywa Coca-Cola, jambo lililovutia
wateja na kuifanya Coca-Cola kuwa sehemu muhimu ya sherehe za Krismasi.
Matangazo haya yalionyesha Coca-Cola kama kinywaji kinachofaa kwa familia
wakati wa sikukuu hi ilipelekea bidhaa hiyo kupedwa zaidi na watu na kuingiza
mauzo zaidi na zaidi kwa Kampuni ya Coca-Cola.
Baada ya mafanikio haya yote Coca-Cola iliendelea kuimarika na kufungua matawi duniani kote, kuhakikisha inawafikia wateja wake katika kila kona ya dunia. Kampuni hii imeendelea kuboresha na kupanua bidhaa zake, ikiwa ni pamoja na kuzindua bidhaa mpya kama Diet Coke na Coca-Cola Zero Sugar, ambazo zimejikita zaidi katika masuala ya afya na matakwa ya wateja wa kisasa. Hata hivyo, muundo wa chupa ya Coca-Cola umeendelea kuwa na sifa yake ya kipekee ya contour, ingawa sasa unatumia plastiki rafiki kwa mazingira. Leo hii, Coca-Cola ni zaidi ya kinywaji; ni alama ya utamaduni inayojulikana popote duniani. Kampuni inaendelea kushikilia nafasi yake kama miongoni mwa kampuni tajiri zaidi duniani, ikiwa na thamani ya soko ya zaidi ya dola bilioni 260. Huu ni ushahidi wa umaarufu na nguvu ya Coca-Cola katika soko la kimataifa, ikiwa ni moja ya alama maarufu zaidi duniani.
Historia Hii imeletwa Kwako kwa Udhamini wa Black D Melody
Unaweza Kutembelea youtube Black D Melody - Nazima Taa - YouTube Kutizama Vimbo Huu
0 Comments